Uzalishaji wa Tafsiri Sadifu katika Matini za Majukwaa ya Kidijiti
PDF

Keywords

Tafsiri
sadifu
majukwaa ya kidijiti

How to Cite

Odawo, M., & Nyandiba, C. (2022). Uzalishaji wa Tafsiri Sadifu katika Matini za Majukwaa ya Kidijiti: Harakati na Changamoto. Nuru Ya Kiswahili, 1(1). Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/1

Abstract

Makala hii inaangazia harakati na changamoto katika kuzalisha tafsiri sadifu katika majukwaa ya kijiditi. Makala inaangazia matini zilizotafsiriwa kutoka lugha chanzi ya Kiingereza kwenda lugha lengwa ya Kiswahili. Uteuzi wa kimakusudi ulitumiwa kupata sampuli sadifu kutoka majukwaa ya tuko.com na bbc.com. Ukusanyaji wa data uliofanywa kwa takriban miezi mitatu: kuanzia Julai hadi Septemba mwaka wa 2018 ulihusu usomaji wa matini ili kudondoa data yakini kupitia rununu na tarakilishi. Matini zilipakuliwa kutoka mtandaoni na kunakiliwa kwenye daftari kabla ya kuchanganuliwa. Utafiti huu umebainisha kuwa wafasiri walijitahidi kuzalisha tafsiri sadifu zenye utoshelevu wa kimaana. Hata hivyo, kwa kiasi kikubwa, harakati hizo za kuzalisha tafsiri sadifu zimekumbwa na changamoto ambazo zimedhihirika kupitia ujitokezaji wa tofauti za kiutamaduni kati ya lugha chanzi na lugha lengwa, uchechefu wa visawe vya kisayansi na kiufundi, tafsiri tenge ya misamiati ibuka na ugumu wa kutafsiri misamiati ya TEHAMA. Makala hii inapendekeza kuwa, pana haja ya kuweka mikakati ya kuboresha tafsiri ya matini tepe zinazotafsiriwa katika majukwaa ya kidijiti ili kuhakikisha usadifu wa jumbe zinazowasilishwa kwa hadhira lengwa katika harakati za kufanikisha mawasiliano timilifu.

PDF