Miktadha ya Matumizi ya U-Nigeria katika Video za Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania
PDF

Keywords

U-Nigeria
kizazi kipya
muziki
nyimbo
muktadha

How to Cite

Kasiga , G. A. (2022). Miktadha ya Matumizi ya U-Nigeria katika Video za Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania. Nuru Ya Kiswahili, 1(2), 184–211. Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/18

Abstract

Tasnia ya Muziki wa Kizazi Kipya wa Kiswahili nchini Tanzania imetekwa na utamaduni wa nje, hususani wa Kinigeria. Hali hii ikiendelea itapoteza utambulisho wa Kitanzania katika sanaa. Kwa hali hiyo, makala imechunguza miktadha ya matumizi ya U-Nigeria katika video za nyimbo za muziki wa kizazi kipya wa Kiswahili nchini Tanzania ili kubaini misukumo yake na kutazama njia za kuupunguza na kuuondosha. Makala imetumia mkabala wa kitaamuli. Data zilikusanywa maktabani na uwandani. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kama kiunzi cha uchambuzi na mjadala. Hatimaye, makala imebaini miktadha saba ya utumiwaji wa U-Nigeria. Miktadha hiyo imehusisha mivuto ya kiubidhaishaji, matumizi ya vyombo vya habari, mivuto ya kiujumi na kibunifu, na mivuto kutokana na mwigo kutoka wasanii nguli. Miktadha mingine imehusisha misukumo ya wasikilizaji na watazamaji, ukosefu wa alama ya utambulisho wa kitamaduni, na ukosefu wa elimu ya tasnia ya muziki. Mwisho, imependekezwa kuwa ili kulinda utamaduni wa Kitanzania kupitia muziki, ni vema wasanii wapatiwe warsha, semina, na madarasa maalumu ya kukuza vipaji vyao kwa maslahi ya jamii nzima ya Watanzania.

PDF