Ufundishaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kupitia Fasihi
PDF

Keywords

Ufundishaji wa Kiswahili
lugha ya pili
fasihi
mtaala wa umahiri

How to Cite

Bikorimana, D. . (2023). Ufundishaji wa Kiswahili kama Lugha ya Pili kupitia Fasihi : Mfano wa Shule Teule za Sekondari Nchini Rwanda. Nuru Ya Kiswahili, 2(2), 25–48. Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/23

Abstract

Elimu ya Rwanda inakabiliwa na changamoto ya kikwazo cha lugha, hasa lugha ya kufundishia. Walimu wanasema kuwa mara nyingi wanafunzi hushindwa kuelewa masomo kutokana na kiwango kidogo cha uelewa na kuwasiliana katika lugha wanazojifunza shuleni (Urunana, 2018). Hali hii imetoa msukumo wa kuibuka kwa makala hii ili kutathmini namna fasihi inavyotumiwa, na inavyoweza kutumiwa katika ufundishaji wa lugha ya pili kwa mazingira yanayotawaliwa na mtaala wa umahiri nchini Rwanda. Utafiti ulioibua makala hii uliegemea katika mkabala wa kitaamuli na kuongozwa na Nadharia Jengaji iliyioasisiwa na Piaget kati ya miaka 1896 – 1980. Mbinu za ukusanyaji data zilizotumika ni mahojiano, ushuhudiaji na uchambuzi matini. Kwa kutumia sampuli lengwa, washiriki wa utafiti walikuwa walimu kumi na tano (15) na wanafunzi sabini (70) wa Kiswahili kutoka shule za sekondari nne zilizochaguliwa nchini Rwanda. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa fasihi huchukuliwa kama somo tu. Walimu na wanafunzi hawajatambua kwamba fasihi inaweza kutumiwa kama nyenzo ya kufundishia na kujifunzia lugha na hawajajua namna ya kuitumia. 

PDF