Msukumo wa Uwasilishaji wa Hisia za Watoto Kupitia Maigizo ya Utotoni
PDF

Keywords

Hisia
Maigizo ya Utotoni
Mtoto
Ung’amuzibwete

How to Cite

Shima, G. . (2023). Msukumo wa Uwasilishaji wa Hisia za Watoto Kupitia Maigizo ya Utotoni. Nuru Ya Kiswahili, 2(1), 86–112. Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/39

Abstract

Makala hii inaeleza msukumo wa uwasilishaji wa hisia za watoto kupitia maigizo ya utotoni. Msukumo wa uwasilishaji wa hisia hizo haujawekwa bayana. Hali hii inachangia kutopewa umakini kwa uwasilishaji na uelewekaji wake (Walton, 1990). Nadharia ya Saikolojia Changanuzi, kupitia msingi wa ung’amuzibwete, imetumika kuongoza mjadala wa makala hii. Msingi huo unaeleza kuwa mawazo na matamanio yaliyomo akilini mwa mtunzi wa kazi za kifasihi, hubweteka na kushindwa kutolewa kwa njia ya moja kwa moja kutokana na sababu mbalimbali. Mawazo ya msingi huo yamesaidia kueleza msukumo unaowafanya watoto wawasilishe hisia zao kupitia maigizo ya utotoni. Data za utafiti uliozaa makala hii zilipatikana kupitia njia ya mahojiano[1]. Mahojiano yalifanywa kwa wazazi/walezi, walimu wa shule za msingi, wahadhiri wa taaluma za fasihi, na watunzi wa kazi za kifasihi za watoto. Makala inaeleza kuwa sababu za kimchakato-makuzi na kidhima-tanzu huwasukuma watoto kuwasilisha hisia zao kupitia maigizo tajwa. Makala inapendekeza kuwa wazazi/walezi, walimu na wadau wengine wanaohusika na watoto wasipuuzie maigizo haya kwa kuwa msingi wa uwasilishaji wake ni mchakato wa ukuaji na sifa ya maigizo hayo.

 

[1] Data hizi zilikusanywa na mwandishi wa makala hii mwaka 2019 kwa ajili ya kukamilisha utafiti wa masomo ya ngazi ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

PDF