Mbinu za Kukabiliana na Utamaushi katika Fasihi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Wimbo Teule wa Jux na Diamond Platnumz na Kazi Teule za Kezilahabi
PDF

Keywords

utamaushi
udhanaishi
Bongo fleva

How to Cite

Malugu, A. A., & Jjingo, C. (2024). Mbinu za Kukabiliana na Utamaushi katika Fasihi ya Kiswahili: Ulinganisho wa Wimbo Teule wa Jux na Diamond Platnumz na Kazi Teule za Kezilahabi. Nuru Ya Kiswahili, 3(1), 27–42. Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/48

Abstract

Makala hii inakusudia kuonesha namna utamaushi unavyojitokeza katika wimbo wa “Enjoy” na kazi teule za Kezilahabi. Kutokana na maisha kuonekana kama kitu cha kukatisha tamaa (kutamausha) kwa kadri yalivyogubikwa na madhila mbalimbali, wimbo wa “Enjoy” unaonesha kuwa suluhisho ni kuamua “ku-enjoy” (kuyafurahia tu) kwa kadri mtu anavyoweza baada ya kupata nafasi ya kufanya hivyo. Hii ni tofauti na ilivyo katika kazi zingine za kidhanaishi, hususani kazi za Kezilahabi, ambazo zinaonesha kuwa suluhisho ni kujiua. Nadharia ya Udhanaishi iliongoza katika uchambuzi wa matini teule. Mbinu ya usampulishaji lengwa ilitumika katika kupata data zilizofanikisha makala hii. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi matini. Matokeo ya utafiti uliozaa makala hii yanaonesha kuwa maisha ayaishiyo mwanadamu ni mafupi, mwanadamu anao uhuru wake binafsi, kuna kukata tamaa kunakosababishwa na masuala ya mapenzi, dunia ni uwanja wa fujo—kila mtu amekuja kufanya fujo zake na mwisho atajiondokea, na, mwisho, masuala ya mahusiano ya kimapenzi ni huzuni tupu. Makala inahitimisha kwa kutoa mapendekezo kuwa suluhu ya kukata tamaa maishani siyo kujiua bali kuyafurahia maisha kwa kadri mtu awezavyo kwani kujiua hakutatui tatizo husika bali huweza kusababisha tatizo ama matatizo mengine. Aidha, iwapo mwanadamu ataamua kufanya fujo zake, ni vema afanye fujo za amani zisizowaathiri wengine. Uhuru binafsi uzingatie mipaka, kwani kila kitu kinapopitiliza huweza kuwa na madhara.

PDF