Riwaya ya Rosa Mistika: Kurunzi ya Malezi ya Vijalunga
PDF

Keywords

malezi
vijalunga
zila

How to Cite

Ponera, A. A. (2024). Riwaya ya Rosa Mistika: Kurunzi ya Malezi ya Vijalunga. Nuru Ya Kiswahili, 3(1), 43–69. Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/50

Abstract

Lengo la makala hii ni kujadili namna riwaya ya Kiswahili inavyosawiri suala la malezi katika familia, hususani malezi ya vijalunga. Makala inaangazia zila za changamoto za vijalunga pamoja na changamoto zenyewe; hatimaye, inapendekeza mikakati ya kuzidhibiti zila hizo. Utafiti na mjadala vimefanywa kwa kutumia Nadharia ya Uhalisia. Data zilikusanywa kwa kutumia njia za uchambuzi wa matini. Matokeo yanaonesha kuwa, kwa jumla, kiini cha matatizo ya vijalunga ni upogo wa malezi wanayoyapata katika familia au asasi za kielimu. Hali hii inasababisha vijalunga kunasa katika zila zinazowazunguka katika maisha yao. Matokeo hayo yamebainisha zila zifuatazo: mabadiliko ya mahitaji ya vijalunga, wazazi au walezi kukosa elimu ya kuishi na vijalunga, pamoja na kupwaya kwa mikakati ya umma kuhusu maisha ya vijalunga. Makala imebainisha kuwa zila hizo zinazaa changamoto zifuatazo: kukosa haki ya malezi, vijalunga kupata ujauzito wakiwa masomoni, kuambukizwa magonjwa, na kutengwa. Kutokana na zila na changamoto zilizobainishwa, mambo yafuatayo yanapendekezwa ili kujenga ustawi wa vijalunga. Mosi, wazazi na walezi wapatiwe elimu ya kuishi na vijalunga. Pili, utoaji wa elimu kuhusu mabadiliko ya mahitaji ya vijalunga uimarishwe. Tatu, mikakati ya umma kuhusu maisha ya vijalunga iimarishwe. Hatimaye, kupitia hoja hizo, tumedhihirisha kuwa riwaya ya Rosa Mistika inafaa kuwa kurunzi ya malezi ya vijalunga ikiwa itasomwa au kufundishwa kwa umakini.

PDF