Nafasi ya Vipindi vya Redio katika Kukuza Fasihi Simulizi ya Watoto
PDF

Keywords

Vipindi vya redio
Watoto Show
Fasihi Simulizi

How to Cite

Ndossa, S. A. . (2022). Nafasi ya Vipindi vya Redio katika Kukuza Fasihi Simulizi ya Watoto: Mifano kutoka Watoto Show. Nuru Ya Kiswahili, 1(1). Retrieved from https://nuru.udom.ac.tz/index.php/journal1/article/view/6

Abstract

Makala hii inajadili mchango wa vipindi vya redio katika kukuza Fasihi Simulizi ya Kiswahili kwa Watoto. Makala hii ni matokeo ya utafiti uliofanyika nchini Tanzania. Utafiti ulikuwa na lengo kuu moja, kuchunguza nafasi ya kipindi cha Watoto Show katika kukuza Fasihi Simulizi ya Kiswahili kwa watoto. Ili kufikia lengo hili, mambo yafuatayo yalifanyika: Mosi, kubainisha muundo wa kipindi cha Watoto Show na namna kinavyotoa fursa kwa vipera vya Fasihi Simulizi ya Kiswahili. Pili, kubainisha vipera vya Fasihi Simulizi vinavyochomoza katika kipindi teule. Tatu, kujadili umuhimu wa vipera hivyo kwa maendeleo ya Fasihi Simulizi ya Watoto. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini, ambapo mtafiti alirekodi na kuchambua vipindi 22 vya watoto ili kubaini mambo mbalimbali yanayohusiana na makala hii. Matokeo yanaonesha kuwa vipindi husika vina mchango muhimu katika kukuza Fasihi Simulizi ya Kiswahili kwa Watoto. Kupitia vipindi husika, watoto hupata fursa ya kujifunza hadithi, nyimbo, misemo, vitendawili, vichekesho, na methali.

PDF